NAFASI 500 ZA KAZI HOUSEMAIDS

 TUNAHITAJI WADADA WA KAZI ZA NDANI


Ajira Connection Tanzania Employment Agency, iliyosajiliwa Mnamo mwaka 2024 June, 18, yenye Makao Makuu yake Mwanza wilaya ya Nyamagana. Inayoendesha huduma za Ajira na Rasilimali watu nchini Tanzania; Ikiwa ni Tanzania Bara, na Tanzania Visiwani, tunapenda kuwatangazia, Vijana wote wa kike waliopo nyumbani tu, na wengineo kuwa tumetoa nafasi za kazi za ndani kwa Mikoa yote ya Tanzania.

Hakikisha Mwombaji si Mwanafunzi, uwe ni raia pia wa Tanzania kwa kuzaliwa. Uwe na Afya njema.

Viwango vya Mishahara.

Mishahara imegawanyika katika pande tatu kulingana na Uchumi wa Familia upande wa Mwajiri au Waajiri husika.

1. Familia ya Uchumi wa Chini.

Kiwango cha Mshahara kwa Familia za Uchumi wa chini ni Tzs. 50,000 - 70,000/= kwa mwezi. Familia ya Mfumo huu inakuwa na Majukumu machache na watu wasiopungua wala kuzidi wawili au watatu hadi wanne (2 au 3 - 4). Wakiwa wawili ni Mume na Mke, au Baba na Mtoto, au Mama na Mtoto. Wakiwa watatu ni Familia ya wazazi wawili na Mtoto Mmoja. Wakiwa wanne, Wazazi 2 pamoja na Watoto 2.

2. Familia ya Uchumi wa Kati.

Kiwango cha Mshahara kwa familia za Uchumi wa Kati ni Tzs. 80,000 - 100,000/= kwa mwezi. Majukumu ya Familia kama hizi yanakuwa ya kawaida. Idadi ya watu (wanafamilia), wanakuwa ni kuanzia wawili hadi wanne. Wakizidi sana Mwisho Watano. Inakuwa na Watu Mchanganyiko, aidha wanaweza wakawa wazazi na watoto, au wazazi Pelee kama ni wawili, au Wazazi, watoto na ndugu.

3. Familia ya Uchumi wa Juu.

Kiwango cha Mshahara wake ni Tzs. 110,000 - 300,000/= kwa mwezi. Majukumu ya Familia hii yanakuwa ya kawaida, ila huhitaji watu wenye elimu kidogo aidha kuanzia Form IV na Kuendelea hadi walio hitimu vyuo. Mfano kwa Mtu aliyehitimu Chuo chochote kuanzia ngazi ya cheti Latina fani yoyote ile yeye hulipwa kiasi cha Tzs. 200,000/= kwa mwezi akiwa anajua kiingereza kidogo cha kuwaelekeza hata watoto kufanya Homework, kuzungumza na watoto wanapotoka shuleni, na hata mara moja moja kama sehemu ya life style ya familia ukawa unazungumza na Wanafamilia. Mara nyingi Familia hizi zinakuwa za waislam kwa asilimia 65% na kwa Wakristo Asilimia 35%

Mfano mwingine kwa wale waliosomea Masuala ya Upishi, Masuala ya Hotel (Hotel Managements, Masuala ya Utunzaji wa nyumba (House Keeping), wao asilimia kubwa hulipwa kiasi cha Tzs. 300,000/= kwa mwezi. Aidha anaweza akawa Mwajiri ni Mtanzania au Raia wa Kihindi (Mhindi), na raia wengineo wenye asili za kigeni wanaoishi nchini Tanzania.

Sifa za Mwombaji wa Kazi.

(a): Awe raia wa Tanzania.

(b): Awe ana akili timamu.

(c): Awe mlezi bora kwa watoto

(d): Awe na Upendo kwa Familia.

(e): Awe Mkristo au Muislam.

(f): Awe na Wadhamini ndugu wa karibu, na Barua zao za kumdhamini. Barua ziwe mbili na kila Barua iwe na Picha (Passport size) ya Mdhamini, na Barua za Wadhamini zikapitishwe na Viongozi wa Serikali za mtaa kwa kuzigongea Mihuri.

(g): Awe na Barua ya Utambulisho toka serikali ya mtaa anapoishi au anapotoka. Barua hii iwe na Picha (Passport size) ya Mwombaji.

(h): Walio na NIDA au Namba za NIDA watawasilisha. Kwa wasiokuwa na NIDA watawasilisha viambatanishi vilivyotajwa katika kipengele ( "f" na "g").

NB.

>Kwa yeyote atakayependa kwenda kufanya kazi Mkoani, Nauli atalipiwa kwa kukatiwa Ticket na Kusafirishwa mpaka eneo la kazi husika katika Mkoa aliopendelea kwenda.

Usalama

Usalama wa Makazi na Kazi ni salama kabisa, hakuna changamoto yoyote ile. Pis taarifa za Waajiri zitatumwa kwa Wadhamini wa wadada (House girls/Housemaids), kwa ajili ya kuziunganisha pande zote mbili na kuwa familia moja.

Jinsi ya Kuomba

Andika Barua yako ya Maombi ya kazi Ukiambatanisha katika Maelezo yako Mkoa au Mikoa unayopendelea kwenda kufanya Kazi. Pia Barua zote ziandikwe kwa Mkono, Ukipendelea kwenda kuchapa ni sawa ila siyo lazima.

Barua zote zitumie Anuani ya Makao Makuu hata kama zitawasilishwa kwa Mawakala wetu waliopo Mikoani, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Geita, Musoma, Magu, Mwanza.

Anuani ya Makao Makuu.

RC/RECRUITMENT CONSULTANT,

AJIRA CONNECTION TANZANIA,

EMPLOYMENT AGENCY,

S.L.P 1995,

MWANZA TANZANIA.

Unaweza wasilisha moja kwa moja kupitia,

Email: ajiraconnectiontz.info@gmail.com

WhatsApp: +255 617 459 447

WhatsApp: +255 685 853 110

Mawasiliano.

Piga/Sms: +255 617 459 447 au +255 784 553 445.


Maoni